Ripoti ya shirika la habari Ahlul Bayt(as)-ABNA- Hadi Al-Amiri Waziri wa ujenzi wa Iraq katika maongezi yake na Televisheni ya Al-Ghadir alisema: Silaha za Saudia Arabia kupitia njia ya Uturuki kuwafikia Waasi wa Syria, kunako suala hili mara kadhaa Marekani ishaongelea kua uagizagi silaha kwa Waasi Syria ni suala lisilokubalika.
Akiendelea kusema: Kubadilika utawala Syria ni hatari kwa Jamuhuri ya Iraq.
Aidha alisema kua Wananchi wa Syria wahitaji mabadiliko na mabadiliko hayo hayawezi kupatikana kwa kuingilia nchi zengine kama Qatar, Saudia Arabia na Uturuki.
Pia alisisitiza kwa kusema: Mabadiliko ya nchi za Kiarabu sasa ni Muamko wa Kiislamu na si kama huitwa mabadiliko haya ni Muamko wa Kiarabu, yote haya ni kutaka kubadili picha nzima ya Muamko wa Kiislamu na kuipa jina lingine.
Akimalizia kwa kusema Bw. Amiri: Fitina zilizosambazwa na Marekani kunako madhehebu ni hatari kwa Umma wa Kiislamu, Marekani afahamu nini kunako Uislamu?!, lengo la Marekani ni kufumba Waislamu macho na kufuta picha nzima ya Muamko wa Kiislamu ila mpaka sasa hajafaanisha kunako suala hilo.